SIRI YA SIMBA KUMPOTEZA TWITE YAFICHUKA

SIRI YA SIMBA KUMPOTEZA TWITE YAFICHUKA

Mbuyu Twite

MAMBO matatu yamemfanya beki Mbuyu Twite wa APR ya Rwanda, aachane na Simba SC na kuamua kujiunga na Yanga SC,  imebainika baada ya uchunguzi wa kina uliohusisha vyanzo kutoka Tanzania, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Mambo hayo ambayo kwa mjumuisho unaweza kuyaita ‘Ujanja ujanja wa mjini’ wa viongozi wa klabu hiyo ndio leo, yanaiponza klabu hiyo kumpoteza aina ya mchezaji ambaye walimuhitaji sana kwenye kikosi chao ili kujiimarisha.
Mosi; Namna ambavyo ‘walimuenzi’ kiungo Patrick Mutesa Mafisango (sasa marehemu), pili; desturi ya kuwaacha wachezaji wa kigeni baada ya kuwasajili, hata kabla hawajaitumikia timu mfano Lino Masombo, Derrick Walullya na wengineo na tatu hadhi ya klabu yao kwa sasa ukilinganisha Yanga na Azam FC.
Habari za kiuchunguzi, ambazo chanzo imezipata zinasema kwamba Mbuyu alilishwa ‘sumu’ za kutosha ili aichukie Simba, kwanza klabu hiyo ilivyoutelekeza mwili wa marehemu Mafisango baada ya kifo chake, ambao hakuna kiongozi mkuu wa klabu hjiyo hata mmoja aliyekwenda kumzika DRC, zaidi ya Mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji na mchezaji mmoja.
Pamoja na namna ambavyo Simba hawakujali kabisa mambo mengine muhimu kuhusu marehemu Mafisango, kama arobaini yake na kadhalika, Wakongo wameichukulia hiyo kama ni dharaua na ulipotokea mjadala Mbuyu aende wapi, watu wa Kongo wakamnyooshea kidole kinachoelekeza Jangwani.
Ikumbukwe, Mafisango aliyejiunga na Simba akitokea Azam FC, iliyomsajili kutoka APR ya Rwanda, alifariki akiwa mchezaji muhimu ndani ya Simba akiongoza kwa kufunga mabao na mwenye mchango mkubwa kwenye timu.
Simba, hivi karibuni ilimsajili mchezaji Lino Masombo kutoka DRC, lakini baada ya mwezi mmoja na ushei ikamtema kama ilivyofanya kwa Mganda, Derrick Walullya msimu uliopita, hilo limetajwa kumsitisha Mbuyu kuangukia Msimbazi na kuamua kurudisha fedha zote alizochukua kwa Mwenyekiti, Ismail Aden Rage (dola za kimarekani 30,000 kwa mujibu wa Simba).
Lakini pia, wakati Mbuyu anasaini Simba kuchukua fedha, alikuwa hajui kwamba katika soka ya Tanzania hivi sasa, klabu ambazo zinachuana kwa ‘utajiri’ ni Habari zaidi bonyeza hapa bongostaz.blogspot

Post a Comment

Previous Post Next Post