TAMASHA LA DINI "LOVE TANZANIA" LILIVYOTIA FORA VIWANJA VYA JANGWANI JIJI DAR.

Pichani Juu na Chini ni Umati wa Watanzania uliofurika kwenye Tamasha la Dini lililopewa jina la LOVE TANZANIA linaloendelea katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam likiongozwa na Askofu Andrew Palau kutoka Marekani.
Vijana walioongoza na Askofu Andrew Palau wakitoa burudani na mafundisho ya dini kwa njia muziki.
Wana Dar es Salaam wakiendelea kumiminika katika viwanja vya Jangwani.
Mmoja wa Wahudumu katika Tamasha hilo akipata chakula cha mchana na familia yake Uwanjani hapo.
Umati wa watu ukiwa kwenye foleni ya kupata huduma ya chakula uwanja hapo.
Moja ya Magari na wafanyakazi wa Kampuni ya Usafi iliyopewa Zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd likiwa limepaki katika Viwanja vya Jangwani kuhakikisha Usafi unazingatiwa Uwanjani hapo wakati tamasha la Dini lililopewa jina la LOVE TANZANIA likiendelea.
Pichani Juu na Chini ni moja ya michezo iliyofanyika kama sehemu ya burudani uwanjani hapo ambapo ilionekana kuvutia Umati wa Watanzania waliohudhuria tamasha hilo.
Vijana, Watoto kwa Wazee wakitazama mchezo wa mapikipiki.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd akihakikisha swala usafi linazingitiwa uwanjani hapo kama inavyoonekana.
Wananchi waliohudhuria tamasha hilo wakishuhudia mchezo wa Baiskeli.
Palikuwa hapatoshi Jangwani.
Ulinzi na Usalama kwa raia ulikuwepo.
Familia zikiendelea kula, kunywa na kufurahi uwanjani hapo.
Hili ni Jukwaa la kimataifa kutoka nchini Uganda maalum kwa ajili ya Tamasha lililopewa jina la LOVE TANZANIA likiongozwa na Askofu Andrew Palau kutoka nchini Marekani, haijawahi kutokea kusikia Sound na Mziki wa Ukweli nchini kwa mliohudhuria tamasha hili mtasema.

Post a Comment

Previous Post Next Post