
Meneja
wa Kinywaji Kipya cha MALTIZA kinachozalishwa na TBL Bi. Consolata
Adam akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na kuzinduliwa kwa
kinywaji hicho kipya kinachopatikana katika ladha mbili za APPLE na PINE
(Pineapple) ambacho amefafanua kwamba Tanzania imekuwa ya kwanza kwa
Afrika kuzindua kinywaji cha aina hiyo kisicho na kilevi chenye ubora
na kinachotengenezwa na kimea halisi kinachozalishwa hapa nchini.
Bi.
Consolata Adam amesema kinywaji hicho kinapatikana katika ujazo wa
330Mls na kimeshasambazwa nchini kote na bei yake ni shilingi 1500,
aliongeza kuwa kinywaji hicho ni halisi kisichotiwa rangi na kuwataka
Watanzania kujiburudisha na MALTIZA.

Bi. Consolata Adam akionyesha kopo za Ujazo wa 330Mls za kinywaji cha MALTIZA aina ya APPLE na PINE
إرسال تعليق