
Manchester City imeweka dau la pauni Milioni 6.2 kwa ajili ya winga wa Swansea, Scott Sinclair mwenye umri wa miaka 23.
Hamburg wamesema watafanya "lolote wawezalo" kukamilisha usajili
wa kiungo wa Tottenham, Rafael van der Vaart, mwenye umri wa miaka 29,
kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
West Ham itajaribu kwa mara ya mwisho kumsajili mshambuliaji wa
Liverpool, Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 23, kabla ya kufungwa kwa
dirisha la usajili na kuwapa fursa Wekundu hao kujaribu kumsajili
mshambuliaji wa Arsenal, Theo Walcott.
Mshambuliaji wa Liverpool, Andy Carroll anajiandaa kuwa nje ya kikosi
cha Wekundu hao kitakachocheza mechi ya Kombe la UEDA dhidi ya Hearts,
habari zaidi zikisema ataondoka katika klabu hiyo.
Post a Comment