FLETCTHER KUCHEZA ULAYA

Dimitar Berbatov, mwenye umri wa miaka 31, sasa anafanya kila
liwezekanalo kuhakikisha anakamilisha uhamisho wake kwenda Fulham kutoka
Manchester United.

Beki wa Tottenham na England, Michael Dawson, mwenye umri wa miaka 28, anaweza kuondoka tu White Hart Lane, licha ya kwamba majeruhi ya Younes Kaboul yanaweza kumuweka nje ya uwanja hadi Krisimasi.
Arsenal inataka kufanya usajili wa ghafla na wa kushitua wa
kiungo wa Chelsea, Michael Essien. Arsene Wenger anamtaka kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 29 kwa mkopo baada ya mambo yake kumuendea kombo
Stamford Bridge.
Mshambuliaji wa Arsenal, Nicklas Bendtner, mwenye umri wa miaka
24, amepewa ofa na Stoke City ya kusajiliwa kwa mkopo, lakini klabu
nyingine kadhaa zinawasiliana na mwakilishi wake.
Chelsea inajiandaa kumtoa kwa mkopo mshambuliaji Daniel
Sturridge, mwenye umri wa miaka 22, kama watafanikiwa kukamilisha
usajili wa mchezaji wa Bayer Leverkusen, Andre Schurrle. Mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 20 anaweza kugharimu pauni Milioni 20.
إرسال تعليق