USAJILI WA NGUVU WAMBAKIZA VAN PERSIE ARSENAL
Santi Cazorla amekutana na wachezaji wenzake wa Arsenal, baada ya kiung
huyo mwenye umri wa miaka 27 kukamilisha vipimo na uhamisho wa dau la
pauni Milioni 20 kutoka Malaga.
MCHEZAJI mpya wa Aston Villa, Ron Vlaar amemshauri mchezaji
mwenzake wa Uholanzi, Robin van Persie asiende Juventus, kwa kuwa ni
mshambuliaji huyo wa Arsenal aliyemvutia yeye kuja kucheza England.
Pia
Arsenal inatumai kwamba Robin van Persie atabaki katika klabu
hiyo, baada ya Mholanzi huyo kuvutiwa na jitihada za kuboresha kikosi
cha Washika Bunduki hao.
إرسال تعليق