![]() |
Charlie Adam akiwa na jezi yake Stoke |
Stoke
City imemsajili kiungo wa Scotland, Charlie Adam kwa dau la pauni
Milioni 4 kutoka Liverpool. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28,
alipokewa na kocha wa Tony Pulis katika Uwanja wa mazoezi wa Stoke leo
asubuhi kabla ya kufanyiwa vipimo afya na kusaini mkataba wa miaka
minne. Pia katika timu ya Hamburg
![]() |
Rafael van der Vaart akiwa na Frank Arnesen |
Kiungo wa
Tottenham, Rafael van der Vaart amerejea Hamburg kwa uhamisho wa pauni
Milioni 10.3. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi, amesaini mkataba wa
miaka mitatu na klabu hiyo ya Bundesliga, baada ya kufuzu vipimo vya afya na kukabidhiwa jezi namba 23 ya kufanyia kazi Imtech Arena.
KARIBU NYUMBANI:
Post a Comment