VICTOR WANYAMA AIBEBA CELTIC, AIFIKISHA KATIKA MAKUNDI

Victor Wanyama

Klabu ya Celtic imefuzu kushiriki raundi ya makundi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minne katika michuano ya kufuzu kwa kombe la klabu bingwa barani ulaya, kufuatia ushindi wake dhidi ya Helsingborgs.
Baada ya kushinda mechi ya kwanza kwa mabao 2-0 nchini Sweden, Celtic, iliimarisha matumaini yake baada ya kufunga bao la tatu kunako dakika ya 30 kupitia kwa mchezaji Gary Hooper.
Celtic yapiga hatua

Katika kipindi cha pili Celtic nusura ipate bao lingine lakini kwaju wa James Forrest uligonga mwamba.
Kipa wa Helsingborgs Par Hansson alikuwa na kazi ya ziada wakati wa mechi hiyo lakini juhudi zake zilifika ukingoni pale Mkenya Victor Wanyama alipochupa na kuifungia Celtic bao lao la pili na kuisaidia Celtic kufuzu kwa raundi ya makundi kwa jumla ya mabao 4-0.

Post a Comment

Previous Post Next Post