KENYA HALI SASA SHWARI BAADA YA GHASIA ZA SIKU TATU

Hali Mjini wa Mombasa nchini Kenya inasemekana kuwa shwari kufuatia
ghasia zilizoanza siku ya jumatatu baada ya kuuwawa kwa kiongozi wa
kidini anayehusishwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab sheikh Aboud Rogo
Mohammed.
Tangu kuuwawa kwa kiongozi huyo kumekuwa na ghasia za hapa na pale
mjini Mombasa, Tayari watu 24 wamefikishwa mahakamani kufuatia ghasia
hizo. Kwa sasa serikali imeunda jopo la watu 11 kuchunguza mauaji ya
Sheikh Rogo na pia ghasia zilizosababisha mauaji ya watu wanne wakiwemo
maafisa watatu wa polisi.
Amina Abubakar amezungumza na mwandishi wetu wa Mombasa Eric Ponda juu ya hali halisi ya mambo kwa sasa
Mwandishi Amina Abubakar
Chanzo:- DW Swahili
Amina Abubakar amezungumza na mwandishi wetu wa Mombasa Eric Ponda juu ya hali halisi ya mambo kwa sasa
Sikiliza mazungumzo kati ya Amina Abubakar na Eric Ponda bofya hapa
Mwandishi Amina Abubakar
Chanzo:- DW Swahili
Post a Comment