WATU 17 WAMEFARIKI NA WENGINE 77 WAMEJERUHIWA VIBAYA KUTOKANA NA AJALI YA BASI LA SABENA


kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Bw.Mohamed Mpinga 
Watu 17 wamekufa papo hapo na wengine kadha kujeruhiwa katika ajali ya basi ya kampuni ya ya Sabena ya mkoani Tabora.

Ajali hiyo ilitokea katika kata ya kitunda jana kufuatia gurudumu la mbele la basi la Sabena kupasuka na kuanguka porini kata ya itunda wilayani sikonge

Majeruhi 77 ambapo kati yao watano hali zao si nzuri na wamelazwa katika hospitali teule ya wilaya ya sikonge .

Basi hilo lilianza safari yake kutokea jijini mwanza kuelekea mkoani mbeya.

Waliokuwa katika ajali hiyo ni pamoja na askari polisi wilaya ya uyui aliyetambuliwa kwa jina moja la Heri

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa imetokea majira ya saa 1 na saa 2 usiku wakati basi hilo likitoka Tabora mjini kwenda Mbeya na kuwa hadi sasa RTO na kamanda wa polisi wa mkoa wa Tabora wamekwenda eneo la tukio ambalo ni umbali wa zaidi ya km 200 kutoka Tabora mjini kuelekea Mbeya

kamanda Mpinga alisema kuwa idadi kamili ya watu waliopoteza maisha hadi sasa ni utata kutokana na taarifa tofauti zilizofika ofisini kwake ambapo taarifa za awali zilidai watu 13 ,taarifa nyingine zinadai watu 16 hivyo alidai taarifa sahihi zitatolewa baada ya RTO na kamanda wa polisi wa mkoa huo kurejea kutoka eneo la tukio.

Post a Comment

أحدث أقدم