"WEMA SEPETU NA JOKATE HAWAFAI KUOLEWA NA MWANANGU" MAMA DIAMOND AFUNGUKA:

 "WEMA SEPETU NA JOKATE HAWAFAI KUOLEWA NA MWANANGU" MAMA DIAMOND AFUNGUKA:


MAMA  mzazi wa  mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Sanura Kassim ‘Sandra’  hatimaye amefungua ukurasa mwingine na kusema kati ya Wema Isaac Sepetu na Jokate Mwegelo, hakuna kati yao anayeweza kuolewa
na mwanaye. 

Chanzo kilicho karibu na familia ya akina Diamond, mwishoni mwa wiki iliyopita kilisema kuwa mama mzazi wa staa huyo anawafahamu Jokate na Wema kupitia vyombo vya habari na kwamba ameshawachunguza mabinti hao na kuona hawafai kuwa wakwe zake.

“Kuna wakati mama Diamond alikuwa anavutiwa sana na Wema lakini baadaye alianza kukasirishwa na skendo zake, kwa Jokate naye ikawa hivyohivyo. 

“Mambo yameenda hivyohivyo, mwisho nikasikia amebadili mwelekeo na kusema wote hawafai,” kilisema chanzo hicho.

Waandishi  wetu walienda hadi  Sinzamori jijini Dar, nyumbani kwa Diamond na mama yake ili kujua msimamo wa mama huyo ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Kama mzazi huwa nina nafasi yangu ya kumshauri mwanangu juu ya maisha ya ndoa na aina ya mwanamke anayetaka kumuoa lakini siwezi kumchagulia mke. Jukumu la kuchagua analo mwenyewe, mimi labda nitampa ushauri tu. 

“Kwanza hao akina Wema na Jokate, mimi sishauri hata mmoja wao aolewe na mwanangu,” alisema mama Sandra ambaye inasemekana aliwahi kuishi nyumba moja na Wema kabla hawajamwagana na Diamond.

Chanzo kingine kilichokuwa kikishuhudia mazungumzo hayo, kilifunguka kuwa mama Diamond hakubaliani na mwanaye kumuoa Jokate wala Wema kwa kuwa wote tabia zao zinafanana, hivyo kuleta taswira rahisi kuwa mke anayemfaa mwanaye si Jokate wala Wema ndiyo maana amemtaka mwanaye kuwa makini sana wakati wa kuchagua mwanamke wa kufunga naye ndoa

Post a Comment

Previous Post Next Post