MKUTANO WA OIC KUFIKIA KILELE CHAKE LEO MJINI MAKKAH

MKUTANO WA OIC KUFIKIA KILELE CHAKE LEO MJINI MAKKAH

Viongozi wa Jumuia ya Ushirikiano wa Kiislamu katika mkutano wa Jumuia hiyo mjini Makkah, Saudi Arabia
Mkutano wa dharura wa Jumuia ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) utafikia kilele chake leo Jumatano katika mji Mtukufu wa Makkah.

Katika mkutano huo, yatajidiliwa masuala kadhaa ya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Mgogoro wa Syria.
Katika kikao cha ufunguzi, mfalme wa Saudi Arabia, Abdullah Bin Abdul Aziz alitoa wito wa kuanzishwa kwa kituo maalumu kwa ajili ya mazungumzo kati ya madhahebu za Waislamu ambacho kitakuwa na makao yake mjini Riyadh. Mfalme Abdullah pia alipendekeza kuteua wajumbe wa kituo hicho kutoka katika mkutano wa kilele.
Mkutano huo utaangazia masuala kadhaa hasa mgogoro wa Syria, ambao katika mkutano wa maandalizi uliofanyika Jumatatu alipendekeza kusimamisha uanachama wa Syria katika Jumuia hiyo.

Hotuba mbili zilitolewa katika ufunguzi. Ya kwanza ilitolewa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, Ekmeleddin Ihsanoglu, ambaye alisisitiza kuhusu haja ya kuulinda umoja wa Kiislamu, akiashria kuwa kwa sasa ulimwengu wa Kiislamu katika hali ngumu na kwamba anasubiri maazimio muhimu ya mkutano huo.

Mzungumzaji wa pili alikuwa rais wa Senegal Macky Sall, akibainisha uzito wa hatua ya sasa na kusisitiza haja ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu.

Post a Comment

Previous Post Next Post