VAN PARSIE ATUA MAN U KWA PAUNDI MILIONI 24. HIVI NDIVTO ANAVYOKARIBISHWA

RASMI. VAN PARSIE ATUA MAN U KWA PAUNDI MILIONI 24
Manchester United imefikia makubaliano ya kumsaini Straika wa Arsenal Robin van Persie kwa dau la Pauni Milioni 24 kwa Mkataba wa Miaka minne.
Uthibitisho huu umerushwa na Tovuti ya Man United ambayo imesema dili hii itakamilika baada ya Van Persie kupimwa afya na kukubaliana maslahi yake binafsi.
Mwezi Julai, Van Persie alitangaza kugomea kusaini Mkataba mpya na Arsenal huku Mkataba wake wa sasa ukiwa umebakisha Mwaka mmoja na Arsenal wameamua kumuuza sasa ili wapate Fedha badala ya kungoja Mwakani ambapo angeondoka bure.
Msimu uliopita Van Persi alifunga jumla ya Mabao 44 katika Mechi 57 alizochezea Arsenal na Nchi yake Holland.

DONDOO za Van Persie akiwa ARSENAL:
ALIJIUNGA: 2004
ADA: £2.75m
MECHI: 278
MABAO: 132
GOLI NYINGI ALIZOFUNGA MSIMU MMOJA: 37
VIKOMBE: Viwili (2004 Ngao ya Jamii na 2004/5 FA Cup)
MISIMU MFULULIZO BILA KOMBE: Seven


Msimu uliopita, Van Persie alitunukiwa Tuzo za Mchezaji Bora wa England mbili moja kutoka kwa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa na nyingine toka kwa Waandhishi wa Habari za Soka na pia ndie alikuwa Mfungaj Bora wa Ligi Kuu England

Post a Comment

Previous Post Next Post