YANGA MEZANI NA OKWI
KLABU
ya Yanga tayari imeanza mazungumzo na mshambuliaji wa Simba SC,
Emmanual Okwi na vyanzo vinasema ameomba mshahara wa dola za Kimarekani
3,000 kwa mwezi ili asaini klabu hiyo, ingawa haijulikani kuhusu mkataba
wake wa sasa na klabu yake, Simba SC.
Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb yupo mjini
Kampala, Uganda akishughulikia suala la mchezaji huyo wa kimataifa wa
Uganda.
Alfajiri
ya leo, http://bongostaz.blogspot.com/ imewasiliana na mwandishi mmoja wa habari za
michezo na burudani nchini Uganda, ambaye amesema kiongozi wa Yanga
aliyekwenda Uganda amefanikiwa kumpata Okwi na wameanza mazungumzo.
“Nasikia
Okwi anataka mshahara wa dola 3,000 na anataka alipwe mshahara wake
wote wa mwaka, aweke benki yeye awe anafanya kazi tu,”alisema
mwandishi huyo wa Uganda.
Okwi
amerejea wiki iliyopita Uganda, baada ya takriban wiki tatu za kuwa
majaribio katika klabu ya FC Red Bull Salzburg ya Wals-Siezenheim,
Austria ambayo hivyo haitamnunua.
Simba ilikuwa ina matumaini ya kupata Euro 600,000 ambazo klabu hiyo, ilikuwa tayari kutoa iwapo Mganda huyo angefuzu majaribio.
Awali,
Simba ilipata ofa ya kumuuza Okwi kwa Sh. Bilioni 2 kwa klabu ya
Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini, lakini mshambuliaji huyo akasema
anataka kwenda Ulaya.
Awali
Olando Pirates ya Afrika Kusini ilimuomba Okwi akafanye majaribio huko
kama angefuzu wangemsajili dau la dola 550,000 kabla ya kuibuka kwa
taarifa za kutakiwa Italia na klabu ya Parma.
إرسال تعليق