YANGA TAYARI WAPO KWA OKWI, AZAM NAO WAMO
Okwi |
EMMANUEL Okwi, wakati wowote anaweza kutangazwa kuwa
mchezaji mpya wa Yanga, ingawa Azam FC nao baada ya kukerwa na kitendo cha
Simba kumsainisha Ramadhan Chombo ‘Redondo’ nao wanamsaka wamsainishe kulipa
kisasi.
Hivi unaposoma habari hii, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb yupo mjini Kampala, Uganda akishughulikia suala
la mchezaji huyo wa kimataifa wa Uganda.
“Ndio, nipo Uganda, nipo Kampala hivi sasa, nakubali Rage (Ismail
Aden, Mwenyekiti wa Simba), alinizidi maarifa Kigali (Rwanda) katika usajili wa
Mbuyu Twite, ila sasa na mimi nataka kulipa kisasi, we subiri tu muda si mrefu
utapata habari,”alisema Bin Kleb, alipozungumza na BIN ZUBEIRY(http://bongostaz.blogspot.com/) kwa simu
dakika chache zilizopita kutoka Kampala.
Alipoulizwa ni kuhusu mchezaji gani, Bin Kleb alikataa
kumtaja, lakini inafahamu kwa sasa hakuna mchezaji ambaye Simba
wanamfuatilia Uganda, zaidi ya mchezaji wao tu, Okwi ambaye alikuwa Ulaya kwa
majaribio ambako amefeli.
Wiki iliyopita, Alhaj Rage alimzidi kete Bin Kleb mjini
Kigali, Rwanda katika kumuwania beki wa APR ya huko, Mbuyu Twite, ambaye amesaini
miaka miwili na SImba SC.
Okwi, licha ya awali kuelezwa kwamba amefuzu majaribio katika
klabu ya FC Red Bull Salzburg ya Wals-Siezenheim, Austria, lakini mwishoni mwa
wiki ilielezwa kwamba, klabu hiyo haitamnunua tena, baada ya wiki tatu za kuwa
nchini humo akijaribiwa.
إرسال تعليق