ZAIDI YA WATOTO 1500 WANUFAIKA NA VF-RAMADHAN CARE & SHARE

Mkuu kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akiwakabidhi baadhi ya watoto yatima mbuzi kwa niaba ya watoto wenzao wa mkoa wa Kigoma,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share  inaendeshwa na mfuko huo,wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Shekhe Hassan Idd Hassan Kaburwa,akimkabidhi msaada wa Madaftari mtoto yatima ambae anasoma kidato cha kwanza Zulpha Ally, wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini Kigoma inayoendeshwa na Vodacom Foundation,wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia kulia ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.

Mkuu kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akiwanawisha maji baadhi ya watoto yatima wa mkoa wa Kigoma kwa ajili ya kuanza kufuturu na  watoto wenzao wa mkoa wa huo,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share  inaendeshwa na mfuko huo,wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Mmoja wa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wa Mkoa wa Kigoma akipokea chakula toka kwa Mkuu kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule,tayari kwa kuanza  kufuturu na watoto wenzake wa mkoa  huo,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share  inayoendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon akiwa na mtoto anaeshi katika mazingira magumu Zulpha Ally wakati wa hafla fupi ya kufuturu na kukabidhiwa misaada mbalimbali mkoani Kigoma kwa watoto yatima iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya  Ramadhan Care & Share

Post a Comment

Previous Post Next Post