![]() |
| Luke McCullough (kulia) akiichezea Manchester United dhidi ya Chelsea |
Luke
McCullough, mwenye umri wa miaka 18, ambaye alikuwa Nahodha wa akademi
hiyo msimu uliopita, alinaswa akimla raha binti huyo mwenye miaka 19
kwenye kamera za CCTV alfajiri ya saa 11:00 Jumatatu baada ya
kutokakujirusha.
Beki huyo wa Ireland Kaskazini, anasifiwa na mabosi wa Old Trafford kuwa 'Jonny Evans mpya'.
Tukio
hilo lililotokea Concert Square, baa moja maarufu Liverpool,
litamchanganya sana Kocha Sir Alex Ferguson, ambaye wiki iliyopita
aliwapiga marufuku wachezaji wake wote wa U23 kuendesha magari mapya ya
kimichezo kutoka kwa wadhamini wao wapya, Chevrolet.
Inadaiwa wawili hao walitoka nje ya mlango kidogo na kuvua nguo nusu kisha kuanza kupelekeshana.
Maofisa
wa Polisi walipowaona wakawazungukia na kuwakamata. Kabinti kaliachiwa
kwanza baada ya kuieleza Polisi ukweli wa tukio, wakati Nahodha wa timu
ya vijana ya Ireland, na beki wa kati alishikiliwa kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa.
Msemaji
wa Jeshi la Polisi Merseyside, alithibitisha kukamatwa kwa kijana huyo
mwenye umri wa miaka 18 na binti mwenye miaka 19 alfajiri ya Jumatatu.
WASIFU WA LUKE MCCULLOUGH
- Kuzaliwa: 15/2/1994, Portadown, N. Ire
- Nafasi: Beki la kati
- Timu ya taifa: Ireland Kaskazini (U17)
- Kujiunga United: 1/7/2010
- Msimu huu: Nahodha Man U Akademi, amecheza mechi 25
- Timu za awali: Dungannon Swifts, County Armagh na Portadown Colleg
Soma zaidi: http://www.dailymail.co.uk

Post a Comment