MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed
‘Shilole’ amepondwa vibaya katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga
Magharibi, Mhe. Kapt. John Komba, baada ya kuvaa kigauni kilichombana na
kumuonyesha maungo yake ya mwili mbele ya viongozi mbalimbali wa
Serikali akiwepo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya
Kikwete.
Mwanamuziki wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiimba pamoja na wasanii wenzake kwenye msiba wa Komba.
Baadhi ya watu waliofika katika Viwanja vya Karimjee vilivyopo Posta
jijini Dar, walianza kunong’onezana baada ya mwanamuziki huyo kujitokeza
mbele na kuimba kipande cha shairi lake huku wakisema kuhusu kigauni
alichovaa bi’dada huyo.
“ Jamani hii aliyovaa si ‘tight’ kabisa, maana yupo tofauti na
wenzake ambao wote wamevaa nguo za heshima zinazowasitiri maumbo yao,
kwa nini yeye ameamua kuvaa hivyo?” alisikika mama mmoja ambaye naye
alikuwemo kwenye maombolezo.
Paparazi wetu alimtafuta Shilole na kumuuliza kuhusiana na hilo
alisema hakuvaa vibaya isipokuwa alionekana vile kutokana na umbo la
mwili wake.

Post a Comment