Sehemu
ya nje ya kituo cha kulelea watoto yatima na wasiojiweza kama
kionekanavyo kwe mbele jioni ya leo,kituo hicho kipo nje kidogo ya mji
wa Tabora,chenye jumla ya watoto wapatao 30 wanaolelewa na kituo hicho.
Mbunge
wa Jimbo la Tabora Mjini,Mh.Aden Rage sambamba na Mkuu wa Wilaya ya
Tabora Mjini,Mh Suleiman Kumchaya wakiwa katika picha ya pamoja na
uwakilishi wa kampuni ya Clouds Media Group sambamba na baadhi ya
Wasanii wa muziki wa Bongofleva ambao usiku huu wanatumbuiza ndani ya
uwanja wa mpira wa Ally Hassan Mwinyi,kwenye tamasha la Serengeti Fiesta
2012,Mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali wa
vyakukula walioutoa kwenye kituo hicho cha ST.Francis

Ofisa
Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Simalenga akimkabidhi Mkuu
wa Wilaya ya Tabora Mjini,Mh Suleiman Kumchaya sehemu ya msaada wa
vyakula uliotolewa na kampuni hiyo kwa kituo cha ST.Francis kilichopo
maeneo ya Ipuli nje kidogo ya mji wa Tabora mjini,anaeshuhudia kulia ni
Mlezi wa kituo hicho Father Anthony Rajesta pia akipokea msaada huo
kwa niaba kutoka kwa mkuu wa Wilaya,Shoto nyuma ya Mkuu wa Wilaya ni
Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini,Mh Aden Rage ambaye pia alijitolea
mipira ya mitano kwa ajili ya michezo ya kituo hicho.
Mkuu
wa Wilaya ya Tabora Mjini,Mh Suleiman Kumchaya akizungumza machache
ikiwemo na kuishukuru kampuni ya Clouds Media Group na wasanii
waliojumuika kwa pamoja katika tukio hilo jioni ya leo,katika suala zima
la kujitolea kuisadia sehemu ya jamii kwa namna moja ama nyingine.
Msanii
mkongwe katika kafika anga ya muziki wa kizazi kipya,Sir Juma Nature
akiwaimbia moja ya wimbo wake watoto wa kituo hicho ambao walionekana
kufurahi kutokana na ujio wa wasanii hao.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya na pia ni muigizaji wa filamu,Shilole
akiwaimbia moja ya wimbo wake watoto wa kituo hicho ambao walionekana
kufurahi kutokana na ujio wa wasanii hao.
Pichani juu ya chini ni sehemuya watoto wanaolelewa na kituo hicho wakiwa na baadhi ya walezi wao.
Picha na michuzijr.blogspot.com

إرسال تعليق