
Na Father Kidevu Blog, Dar es Salaam.
MIKAKATI
na kampeni za majitaka zenye lengo la kumchafua Mbunge wa Jimbo la
Busega mkoani Simiyu, Dk. Titus Kamani, zimeanza kubainika kwa
kumhusisha na tena na tuhuma za mauaji.
Dk. Kamani, ambaye ni miongoni mwa wanachama wa CCM waliojitosa kuwania nafasi ya
Mwenyekiti
wa Mkoa mpya wa Simiyu, ameanza kuchafuliwa akihusishwa na tuhuma za
kutaka kumuua aliyekuwa mbunge wa Busega, Dk. Raphael Chegeni.
Hata
hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, aliwahi
kueleza bayana kuwa wamefanya uchunguzi wa kina na kubaini Dk. Kamani
hahusiki na tuhuma hizo na kwamba, waliotuhumiwa wameshafikishwa
mahakamani.
“Hatumtafuti
Dk Kamani, tukimhitaji tutampata lakini katika uchunguzi wetu
tumebaini tuhuma hizo hazimuhusu," alikaririwa Kamanda Barlow baada ya
kuibuka kwa uvumi kuwa mbunge huyo alikuwa akisakwa na polisi.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es
Salaam, jana, Dk. Kamani amesema kumekuwepo na kampeni chafu za
kuhakikisha jina lake linachafuka ili kudhoofisha harakati zake za
kukitumikia Chama.
Amesema
kuwa tangu alipojitosa kuwania nafasi hiyo, kumekuwepo na mikakati ya
kumchafua inayofanywa na baadhi ya wanasiasa wakiwemo waliopo ndani ya
CCM na kwamba, hilo
amelibaini na atalifikisha kwenye vikao husika.
Dk. Kamani katika taarifa yake amesema kuwa, mbinu chafu hizo zimekuwa zikisukwa na
wanasiasa hao kwa lengo la kumchafua na kumchonganisha na wapigakura wake pamoja na jamii imuone kuwa hafai.
“Makovu
na visasi vya kushindwa katika uchaguzi uliopita kamwe havitaiharibu
Busega wala kunidhoofisha kuwatumia wananchi wangu. Nafahamu hizi ni
mbinu chafu kwa ajili ya kuniharibia katika harakati zangu za kuwania
nafasi ndani ya Chama," alisema katika taarifa hiyo.
Tayari watu wanaotuhumiwa kuhusika katika njama za kutaka kumuua Dk. Chegeni
wameshapandishwa kizimbani kujibu mashitaka hayo.
إرسال تعليق