![]() |
| Vimwana Miss Temeke |
Benny Kisaka,
Mkurugenzi wa BMP Promotions, waandaaji wa Miss Temeke 2012, amesema leo kwamba, katika mlolongo huo wa zawadi, mshindi wa kwanza
atajinyakulia fedha taslim Sh. Milioni 1, wa pili Sh. 800,000, wa tatu Sh. 700,00
sambamba nguo ya kutokea jioni na viatu, vyenye thamani ya Sh. 500,000 kila
mmoja kwa wote watatu.
Kisaka alisema
kwamba duka la kisasa la Mariedo Boutique itatoa gauni la Sh.350,000 na kiatu
cha Sh 150,000 kila mmoja kwa washindi hao watatu wa kwanza watakaoshinda. Alisema
mbali ya washindi hao, mshindi wa nne atajinyakulia kitita cha Sh. 400,000
ambapo mshindi wa tano ataondoka na Sh
300,000 wakati warembo wengine wote watakaosalia kila mmoja atapata Sh.200.000.
Ikiwa ni
funga dimba ya mashindano ya urembo ya kanda nchini, shindano hilo litanogeshwa
na wasanii wanaong’ara katika luninga, Mpoki wa kundi la Komed Original na
Steve Nyerere ambaye mbali ya kuigiza sauti za watu mbalimbali, pia ametoa
filamu kadhaa kwa siku za hivi karibuni.
Mbali ya
wasanii hao, bendi ya Mashujaa Musica,yenye wanamuziki nguli kama Charles Baba,
MCD, Ferguson, Ali Akida sanjari na wanennguaji kama Lilian Internet na
wengineo pia itanogesha usiku huo.
Taji la
Redd's Miss Temeke, linashikiliwa na mrembo Husna Twalib. Warembo wa Miss
Temeke wamekuwa wakijifua kwa wiki tatu sasa chini ya ukufunzi wa Leyla Bhanji,
ambaye amekuwa akisaidiwa pia na warembo wa miaka ya nyuma wa Miss Temeke
akiwemo, Regina Mosha(20020, Hawa Ismail(2003), washiriki wa mwaka jana Joyce
Maweda, Mwajabu Juma, Cynthia Kimasha na katika shoo wamekuwa na Dickson Daud
kutoka kundi la THT.
Shoo ya
ufunguzi itakuwa tofauti kabisa na shoo nyingine yeyote iliyowahi kuyanyika
nchini, kwani imezingatia zaidi urembo na nini msichana anatakiwa kufanya na si
unenguaji tu. Warembo 15 wanatoka katika vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na
Chang'ombe ambapo kila sehemu wametoka warembo watano ambapo washindi watatu wa
kwanza watapata fursa ya moja kwa moja kushiriki Redds Miss Tanzania 2012.
Warembo hao
ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine
Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph,
Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam
Ntakisivya na Esther Albert.
Mbali ya
Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na City Sports Lounge, Jambo Leo,
Mariedo Boutique, Global Publishers, Dodoma Wine, Push Mobile, Mariedo Boutique, 100.5 Times FM, Kitwe
General Traders, Fredito Entertainment, katejoshy.blogsport.com na 88.4 Cloud's
FM.
Temeke
imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo Happiness
Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy Baham mwaka 2003 na
Genevieve Mpangala. Lakini pia imetoa warembo waliowahi kushika nafasi ya pili
na tano bora katika Miss Tanzania kama Jokate Mwegelo, Irene Uwoya, Irene Kiwia,
Queen David, Cecylia Assey, Sabrina Slim, Miriam Odemba, Ediltruda Kalikawe na
Asela Magaka

Post a Comment