Fid Q afikiria kuwapeleka kortini Orijino Komedi kwa kumchafua

Baada ya Orijino Komedi kumshutumu rapper Fareed Kubanda aka Fid Q kuwa amecopy na kupaste beat ya wimbo wake Danger, rapper huyo hajaridhika na hatua zilizochukuliwa mpaka sasa kiasi cha kufikiria kutafuta mwanasheria ili
awaburuze kortini waigizaji hao.
“Looking for a good lawyer dealing with defamation of character cases.. Contact us for details,” Fid alitweet jana.
Baada ya kuona tweet hiyo, Mchakato wa kumpata fid ulifanyika na alipigiwa simu rapper huyo kutaka kujua kama kweli amedhamiria kulipeleka suala hilo kwenye sheria na yeye kusema kuna watu walimshauri afanye hivyo lakini ameamua kupuuzia.

Post a Comment

أحدث أقدم