Hapa bajaji iliyombeba majeruhi ikipita karibu na daladala iliyomgonga mkazi huyo
Huyu ni dereva wa daladala iliyomgonga mkazi huyo akijiandaa kukimbia kabla ya kukamatwa
Hapa akiwa katika usafiri wa Bajaji tayari kukimbizwa Hospitali
mkazi mmoja
wa jijini Dar es Salaam ambaye jina halijaweza patikana mara moja
amenusurika kifo baada ya kugongwa na daladala yenye namba za usajili
T710 ALV linalofanya safari zake kati ya Posta na Mwananyamala .
Ajali hiyo
imetokea majira ya saa 11.30 jioni wakati mkazi huyo akijaribu kuvuka
barabara kutoka eneo la Mahakama kuu kuelekea kituo cha polisi cha
Askari wa wanamaji ufukweni wa bahari ya Hindi.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani wamefika eneo la tukio na kumchukua majeruhi huyo kwa usafiri wa Bajaji na kumpeleka Hospitali kwa matibabu zaidi huku dereva wa Daladala hilo akikamatwa
Habari/Picha na:- http://audifacejackson.blogspot.com
Post a Comment