
Mda huu nimeamua
kuja mitaa hii ya Morocco Bagamoyo Rd kuja kusherehekea sikukuu yangu
ya kuzaliwa na watoto hawa wa mtaani wanaoishi maeneo haya na kila siku
huwa nawaona hapa na wanalala hapa hadi mida ya usiku huwa nikisimama
kwenye mataa huwa wananitambua na kunisalimia so nikaona sio mbaya leo
niwanunulie keki na juice ili tuje kusherehekea kwa pamoja kumbukumbu
hii yangu ya kuzaliwa leo. Najisikia mtu wa furaha sana kuwa na hawa
vijana kwa sababu kila siku nawaona na mungu anaendelea kuwapa pumzi kwa
kuwa na afya nzuri kwa kipato kidogo wanachokipata na mimi nikaona kwa
kidogo nilicho nacho niende kukaa nao wajisikie nao watu kati ya wale
watu.

إرسال تعليق