Jackline Wolper - "Nampenda Sana Dallas kamwe hatutaachana"


Jackline Wolper
WAKATI baadhi ya vyombo vya habari vikidai msanii JacklineWolper ameachana na mchumba wake ambaye ni Dallas, Wolper ameamua kuvunja ukimya na kudai kuwa kamwe hawezi kutengana na mpenzi wake huyo kwani ni mtu ambaye kwa upande fulani anaendesha maisha yake ya kila siku.

Wolper inadaiwa kuwa awali alitaka kuachana na mchumba wake huyo ingawa habari hizo hazikuwa na ukweli wowote, na alipozungumza na mwandishi wa DarTalk, alidai mapenzi yake na Dallas ni kufa na kuzikana hivyo wale wanaosema mabaya juu yake hawana nafasi na wanajisumbua.

“Kwanini niachane na Dallas unajua mapenzi si kitu cha mchezo nampenda sana Dallas na hata yeye pia ananipenda, hivyo si dhani kama kunaweza kutokea kitu kingine cha ajabu eti kwa sababu ya watu wanataka tuachane hatuwezi kamwe.” alidai.

Hata hivyo aliongeza Dallas hajampenda yeye kwa sababu ni mrembo au maarufu ni mapenzi aliyonayo kwake ingawa anakanusha baadhi ya maneno mengine kuwa amempenda jamaa huyo kwa sababu anamshiko mchafu

Post a Comment

أحدث أقدم