
Kamanda
mkuu kikosi cha usalama barabarani Mohamedi mpinga (Kushoto) akipokea
Tshirt kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde zitakazotumika
katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani
inayofanyika kitaifa mkoni Iringa ambapo Airtel ni wadhani wakuu.
Makabithiano hayo yalifanyika katika ofisi za makao makuu ya polisi
usalama barabarani jijini Dar es saalam,akishuhudia ni Mkaguzi msaidizi
wa polisi Inspector Deus Sokoni, madhimisho ya wiki ya Usalama
barabarani yanaanza kesho jumatatu.
*********
· Maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika mkoani Iringa viwanja vya Samora
· Airtel yakabidhi Fulana zenye Ujumbe maalum kwaajili ya kuhamasisha usalama barabarani
Kampuni
ya simu za mikononi ya Airtel imeendeleza dhamira yake ya
kushirikiiana na jeshi la polisi usalama barabarani katika kuhakikisha
ajali za barabarani zinapungua na kudhibitiwa.
Wiki
ya nenda kwa usalama barabarani inafunguliwa kitaifa mkoani Iringa
katika viwanja vya Samora kuanzia tarehe 17-22 mwezi Septemba ambapo
mgeni rasmi anatarajiwa kuwa WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MHE. DKT. EMMANUEL
NCHIMBI kwa niaba ya Mh, Raisi Jakaya Mrisho Kikwete
Akizungumza
na wakati wa hafla maalum ya makabidhiano ya Fulana Ofisa Uhusiano wa
Airtel Jane Matinde alisema "Airtel tunaona ni haki na ni sawa
kuendelea kuthamini usalama barabarni na tunayo dhamira thabiti ya
kuhakikisha tunaelimisha na kuhamasisha jamii na waendesha vyombo vya
moto kuzingatia na kutii sheria za usalam barabarani, hivyo basi
tunaomba watanzania kuunga mkono jitihada hizi ili kuhakikisha kwamba
vyombo vya moto zinakaguliwa na kubandikwa stika maalumu za nenda kwa
usalama barabarani"
Airtel
inadhamini kampeni hii kwa miaka 4 mfululizo ambapo mwaka huu mbali na
kuchapisha stickers imejitolea fulana 800 zenye thamani ya Tsh 8
zilizo na ujumbe maalumu kwa mwaka huu usemao“ Pambana na ajali za
barabarani kwa vitendo, zingatia sheria” makabidhiano hayo yamefanyika
katika ofisi za makao makuu ya polisi usalama barabarini jijini Dar es
saalam.
"Airtel
Tanzania imeamua kuunga mkono kampeni hii ya nenda kwa usalama
barabarani kwa sababu ya ongezeko kubwa la ajali za barabarani ambazo
zinaathiri wateja wetu, aliongeza Bi Mtinde
Bado
Airtel haitaishia hapo tayari tumeshajipanga kufanya kampeni
mbalimbali zitakazokuwa zikitoa elimu kwa watumiaji wa barabara hasa
waenda kwa miguu na madereva wa vyombo vya moto kwa lengo la kupunguza
ajali barabarani huku tukishirikiana na jeshi la polisi usalama
barabarani. alimaliza kwa kusema
Nae
kamanda Mkuu wa Usalama Barabarani Mohamedi Mpinga alisema
"Ninawashukuru sana Airtel kwa ushirikiano wenu katika mkakati wetu wa
kupunguza ajali barabarani, hadi sasa maandalizi yote ya wiki ya nenda
kwa usalama yamekaa sawa na nawahamasisha sana wananchi wote wajitokeze
katika vituo vyetu vyote nchini ili waweze kukagua magari yao na
kujipatia stika za usalama barabarani.
Kwa
mkoa wa Iringa ambapo ndiko tunafanya maadhimisho ya Usalama
barabarani pia tutafanyia ukaguzi pale katika viwanja vya Samora
vilevile kituo cha polisi kati maeneo ya sokoni, kituo cha checkpoint
ivumbilo na kile cha mafinga, alimaliza kwa kusema Kamanda Mpinga.
Post a Comment