MAGAZETI ULAYA LEO HII:- ARSENAL NA UHABA WA MATAJI,FULHAM,LIVEPOOL,TOTTENHAM

ARSENAL IKASAKE MATAJI KWENYE WAVU

Arsenal haijashinda taji lolote kwa zaidi ya miaka saba na klabu hiyo imeambiwa iwapeleke baadhi ya wachezaji wake kwenye mchezo mpya, mpira wa wavu ili kumaliza ukame wa mataji.
Fulham inaweza kumuuza Mousa Dembele kwa Tottenham katika dirisha dogo, lakini mashabiki wa Cottagersmuda si mrefu wataendelea kuimba jina la mchezaji huyo tena, baada ya mmoja wa wachezaji wake wa akademi, ambaye pia anaitwa Mousa Dembele - kufunga hat-trick katika timu ya U18 ya klabu hiyo, dhidi ya Crystal Palace.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers anaweza kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Wekundu hao, Michael Owen baada ya kushuhudia ubutu wa safu yake ya ushambuliaji, wakati wakichapwa mabao 2-0 na Arsenal Uwanja wa Anfield jana.
Tottenham iko tayari kuwaruhusu makipa Carlo Cudicini, mwenye umri wa miaka 38, na Heurelho Gomes mwenye miaka 31 kwenda klabu za Daraja la Kwanza kwa mkopo, baada ya wawili hao kupoteza namba mbele ya kipa Mfaransa, Hugo Lloris mwenye umri wa miaka 25 kutoka Lyon.
 
Sunderland pia imewasiliana na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, Owen, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru, baada ya kutemwa na Manchester United mwishoni mwa msimu.
Habari kamili: Metro

Post a Comment

Previous Post Next Post