ARSENAL IKASAKE MATAJI KWENYE WAVU
Arsenal haijashinda taji lolote kwa zaidi ya miaka saba na klabu
hiyo imeambiwa iwapeleke baadhi ya wachezaji wake kwenye mchezo mpya,
mpira wa wavu ili kumaliza ukame wa mataji.
Fulham inaweza kumuuza Mousa Dembele kwa Tottenham katika dirisha dogo,
lakini mashabiki wa Cottagersmuda si mrefu wataendelea kuimba jina la
mchezaji huyo tena, baada ya mmoja wa wachezaji wake wa akademi, ambaye
pia anaitwa Mousa Dembele - kufunga hat-trick katika timu ya U18 ya
klabu hiyo, dhidi ya Crystal Palace.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers anaweza kumsajili
mshambuliaji wa zamani wa Wekundu hao, Michael Owen baada ya kushuhudia
ubutu wa safu yake ya ushambuliaji, wakati wakichapwa mabao 2-0 na
Arsenal Uwanja wa Anfield jana.
Tottenham
iko tayari kuwaruhusu makipa Carlo Cudicini, mwenye umri wa miaka 38,
na Heurelho Gomes mwenye miaka 31 kwenda klabu za Daraja la Kwanza kwa
mkopo, baada ya wawili hao kupoteza namba mbele ya kipa Mfaransa, Hugo
Lloris mwenye umri wa miaka 25 kutoka Lyon.
Sunderland pia imewasiliana na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka
32, Owen, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru, baada ya kutemwa na
Manchester United mwishoni mwa msimu.
Habari kamili: Metro
إرسال تعليق