MAGAZETI ULAYA LEO HII:- NANI KUONDOKA MAN U, STEFAN OAKES,FRAIZER, SOMA

Jermaine JenasTottenham iko tayari kumto kwa mkopo kiungo wa England, Jermaine Jenas, mwenye umri wa miaka 29, akacheze Daraja la Kwanza ili kujihakikishia nafasi ya kucheza mechi.

Hull City na Huddersfield zote zina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Sunderland, Fraizer Campbell kwa mkopo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alipandishwa kucheza Ligi Kuu akicheza kwa mkopo Hull mwaka 2008.
Stefan Oakes, mwenye umri wa miaka 33, kiungo ambaye alishinda Kombe la Ligi akiwa na Leicester City na kucheza mechi zaidi ya 60 za Ligi Kuu, anaweza kutimkia Spalding United, ambayo inachesa Ligi Kuu ya United Counties.
Stefan OakesMshambuliaji Nicklas Bendtner, mwenye umri wa miaka 24, ambaye amesajiliwa Juventus kwa mkopo wa msimu wa muda mrefu kutoka Arsenal wiki iliyopita, ameambiwa hayuko katika hali nzuri kimchezo ya kuchezea Kibibi Kizee hicho cha Turin.
Mshambuliaji wa Manchester United, Josh King, mwenye umri wa miaka 20, ameionya klabu hiyo kwamba yupo tayari kuondoka Januari kama hatapata nafasi ya kucheza japo mechi kadhaa.
Zenit St Petersburg inatumai kukamilisha usajili wa pauni Milioni 25 wa winga wa Manchester United, Nani, mwenye umri wa miaka 25, kabla ya kufungwa pazia la usajili la Urusi leo.

Post a Comment

Previous Post Next Post