TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Meja Jenerali Samuel Albert Ndomba kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Aidha,
Rais Kikwete amempandisha cheo Meja Jenerali Ndomba kuwa Luteni Jenerali.
Taarifa
iliyotolewa leo, Ijumaa, Septemba 21, 2012, mjini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais –
Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo unaanza leo.
Taarifa
hiyo ya Balozi Sefue imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Meja Jenerali Ndomba
alikuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Jenerali
Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahman A. Shimbo ambaye amestaafu Jeshi kwa mujibu
wa sheria baada ya kufikisha umri wa miaka 60.
Taarifa
ya Balozi Sefue pia imesema kuwa Rais Kikwete amemteua Brigedia Jenerali
Raphael Mugoya Muhuga kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia leo, Ijumaa,
Septemba 21, 2012.
Aidha,
Rais Kikwete amempandisha cheo Brigedia Jenerali Muhuga kuwa Meja Jenerali.
Kabla ya
uteuzi wake, Brigedia Jenerali Muhuga alikuwa Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
21
Septemba, 2012
إرسال تعليق