
Mwaka
huu umekuwa wenye baraka tele katika nchi yetu ya Tanzania kwani mara
ya kwanza tumeona Diamond Platinum juzi juzi tu alikuwa ndani ya
Washington Dc nchini marekani kwa kupiga show yake,mara ya pili tukaona
Martin Kadinda ambaye anahusika na mambo ya fashion designer alipata
mwaliko Neywork city.Sasa habari nzuri ni kwamba Peter msechu naye ndani
ya Chicago.Msanii huyu alifunguka na kusema kwamba yeye ameenda kwa
kupiga show kadhaa pamoja na vitu vyake binafsi kwani msanii huyu ana
mchakato wa kufunguka band yake kwa hiyo huku ameenda kwa kuulizia bei
ya vifaa ambavyo ataweza kufungulia band yake.Pia alisema kwamba atakaa
kama miezi 6 nchini humu mpaka mambo yake yakamilike ndipo atarudi
nchini Tanzania.

Hii ni moja kati ya picha ambayo msanii huyu alipiga akiwa katika maeneo ya Downtown Chicago.

Peter Msechu akiwa na rafiki yake katika maeneo ya millenium park chicago.
Post a Comment