
.
Ni siku chache zimepita toka
rapper Rick Ross kutoa video ya ‘hold me back’ aliyoishoot Nigeria
ambapo ndani yake kumeonyeshwa maisha mabovu wanayoishi Wanigeria.
Ni video ambayo hata kwenye
mitandao ya kijamii asilimia kubwa ya waafrika hasa Wanigeria wameiponda
na moja kati ya mambo ambayo yamewaudhi ni kitendo cha Rick Ross
kuonekana akiwapa watoto dola za kimarekani.
Rapper M.I amekua staa wa
Nigeria wa kwanza kujitokeza na kuiponda hiyo video kwamba mgeni kama
Rick Ross hajui chochote kuhusu historia na maisha ya Wanigeria,
ameivalisha nchi picha mbaya.
Kwenye line nyingine M.I
amesema huko ni kuivunjia nchi heshima ndio maana hajaifurahia kabisa
hiyo video na isitoshe Rick Ross alikua na uwezo wa kuonyesha maeneo
mengine na siyo hizo picha mbaya tu.
Kama hujapata nafasi ya kuichek hiyo video ya Rick Ross ichek hapo chini.
Post a Comment