Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo,(kushoto) na
Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula Raymond Wigenge.
----
MKURUGENZI
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa(TFDA,Haiiti Sillo
amesema kwamba kamati maalum inayoaandaa rasimu za awali ya mifumo
wa kuoanisha usajili wa dawa katika nchi za Afrika Mashariki(EAC)
imeshaanza kazi hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika kipindi cha miaka
miwili ijao.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi huyo wakati akizungumza na waandishi
wa habari katika mkutano wa Ushirikiano wa wafanyabiashara wa kutoka
nchini China na Tanzania kuhusiana na kampuni hizo uliofanyika kwenye
hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dares Salaam.
Mkutano
huo wenye lengo la kutoa elimu kwa wanaotaka wafanyabiashara hao
kutoka nchini China wanaotaka kuwekeza katika sekta hiyo.
“Nchi
za EAC zinategemee dawa nyingi kutoka nje . Rasimu hiyo itasaidia
kuongeza ushirikiano wa kudhibiti dawa bandia kwa pamoja,” . utaratibu
huu utakuwa na msharti yanayofanana katika nchi zote ,alisema Sillo.
Alisema mifumo hiyo itasaidia kupunguza gharama za usajili wa dawa na kuwezesha wananchi kupata dawa zilizo bora na uhakika.
Sillo
aliwataka waombaji wa kusajili kampuni za utengenezaji dawa na vifaa
tiba kuaandaa maelezo yanayotosheleza katika kukidhi viwango vya
ubora na usalama wa bidhaa hizo ili kuepusha ucheweleshaji wa usajili
huo.
“
Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni waombaji wa usajili wa
kampuni hizo kutokidhi viwango vya ubora na usalama wa bidhaa hizi.
Hivyo ninapenda kuchukua nafasi hii kuwataka waombaji wahakikishe kuwa
kabla ya kuwasisilisha maombi ya usajili wahahakikishe maelezo yao
yanajitosheleza,” alisema.
Alizitaja
changamoto nyingine ni kuwa kutokuwepo kwa watafiti wa kutosha
kutathimini ubora na usalama wa dawa , hata hivyo alisema suala hilo
wanalifanyia kazi ili kuongeza rasilimali watu ya kutosha. Changamoto
nyingine ni kutokuwepo kwa ripoti za kuonyesha dawa zilizoleta matatizo
kwa watumiaji kutoka kwa watoa huduma za afya na watengenezaji wa
dawa hizo.
Awali
akifungua mkutano huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,
Regina Kikuli Sillo aliwataka wafanyabiashara hao kuunda mtandao
utakaowasaidia kubadilishana uzoefu katika sekta hiyo.
Naye
Makamu wa Rais wa Chama cha wafanyabiashara wa uingizaji na
usafirishaji wa bidhaa hizo kutoka nchini China, Meng Dongping alisema
wanatengeneza bidhaa hizo ambazo ni bora na kwa gharama nafuu
ukilinganisha na nchi nyingine zilizoendelea.
Aliongeza
kuwa Tanzania ni nchi ya 11 katika ushirikiano wa kibiashara wa bidhaa
hizo barani Afrika na nchi ya pili kwenye soko la bidhaa hizo kwa
upande wa nchi za EAC.
Makamu
Rais huyo aliongeza kuwa, katika kipindi cha miezi sita cha mwaka
2012 ukuaji wa soko bidhaa hizo nchini Tanzania ,umefikia dola za
Marekani milioni 32.61 sawa na asilimia 47
Post a Comment