
VODACOM YAZINDUA BONGA TARIFF YAPUNGUZA 50% YA BEI ZA KUPIGA SIMU KWENDA MITANDAO YOTE
- Wateja wanaweza kupiga simu kwa Tsh1.5.
- Kwenda mitandao yote nchini – kwa siku nzima, kila siku.
Dar e salaam 19th 2012 Kampuni ya Mawasiliano ya
Vodacom Tanzania kuanzia jana,Imeamua kuwafurahisha Wateja wao kwa
kuendelea kuwaboreshea huduma mbalimbali hasa wale wanaotumia simu za
mikononi, wanazo sababu za kuufurahia mtandao wao na kuendelea kupiga
simu zaidi kutokana na mtandao wao kupunguza bei za kupiga simu kwenda
mitandao mingine kwa asilimia 50. Huduma hii mpya ya Bonga tariff inayowezesha wateja kupiga simu kwenda mitandao yote Tanzania kwa Tsh 1.5 kwa sekunde.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Rene Meza,
alisema anapenda kuwajulisha watanzania na wateja wote kwa ujumla kuwa
kwa ajili ya kujiunga na huduma hii mpya, wateja wanatakiwa kupiga
*149*01# na wataunganishwa bure bila malipo yoyote,Hata hivyo wateja wa
Vodacom wataendelea kunufaika na huduma nyingine kama vile vifurushi
vya cheka ‘cheka bundles’
“Kwa mara ya kwanza Tanzania,Mteja akiwa na huduma ya Bonga ahitaji
kubadilisha SIM kadi yake au kubeba simu mbili,kwani bei/huduma ya Bonga
inamwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote ule na kumpunguzia
mteja usumbufu.alisema Meza.
“Tunaishi katika Dunia ambayo inahitaji kila mtu awasiliane na
mwenzake na pia wapendwa wao kwa hivyo ni muhimu kuwawezesha kuwasiliana
kwa bei nafuu na kwa urahisi zaidi,” alisema Meza na kuongezea, “Bonga
itawawezesha Watanzania kuweza kuwasiliana zaidi na kuunganishwa popote
pale walipo na kuweza kuinua
Post a Comment