![]() |
| Wayne Rooney alikosa mechi mbili za England kwa kuwa majeruhi |
Wayne
Rooney anaweza kurejea katika kikosi cha Manchester United leo usiku
ikimenyana na Galatasaray katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mshambuliaji huyo alitarajiwa kuwa nje hadi Oktoba baada ya kuumia kwenye mechi dhidi ya Fulham, Agosti 25.
![]() |
| Rooney anaweza kustaajabisha watu leo kwa kushiriki mechi na Galatasaray |
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, aliumia sana mguu wake wa kulia alipogongwa na Hugo Rodallega wa Fulham, lakini Rooney
amepatiwa tiba nzuri na wataalamu wa tiba wa United na amepona kiasi
kwamba kwa siku tano amekuwa akifanya mazoezi, limeripoti The Sun.
Na Rooney anaweza hata kuanzia benchi katika mechi ya ufunguzi ya United ya Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Old Trafford leo.
Mshambuliaji
huyo wa England kwa uhakika zaidi atakuwepo kwenye mechi ya Jumapili ya
Ligi Kuu dhidi ya Liverpool Uwanja wa Anfield.
SOMA ZAIDI: http://www.dailymail.co.uk


Post a Comment