SAMATTA, ULIMWENGU WAIPAISHA MAZEMBE AFRIKA

SAMATTA, ULIMWENGU WAIPAISHA MAZEMBE AFRIKA

Samatta

MBWANA Samatta amefunga bao moja jioni kwenye Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi, wakati timu yake Tout Puissant Mazembe ikiilaza Al Ahly mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi B, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Samatta alifunga bao hilo dakika ya 49, baada ya pasi nzuri ya Tressor Mabi Mputu, kabla ya D. Kanda kufunga la pili dakika ya 61, pasi ya Mputu tena. Thomas Ulimwengu aliingia dakika ya 67 kuchukua nafasi ya Kanda.
Mbwana ni mchezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Mazembe kwa mwaka wa pili sasa, lakini Ulimwengu alipandishwa kikosi hicho kwa mara ya kwanza mwezi uliopita, baada ya kukaa kikosi cha wachezaji wa akiba tangu asajiliwe katikati ya mwaka jana na leo amecheza mechi ya kwanza.
Mazembe imefikisha pointi10, baada ya kucheza mechi tano, kushinda tatu, sare moja na Berekum Chelsea na kufungwa moja na Al Ahly ugenini,
Al Ahly iliyotoa sare ya 1-1 na Berekum Chelsea nchini Ghana katika mechi yake iliyopita, bado inaongoza kundi hilo kwa pointi zake 10, wakati wababe wapya wa Ghana wanashika nafasi ya tatu kwa pointi zao sita baada ya kutoka sare na Zamalek 1-1, ambao wanashika mkia wakiwa na pointi moja. 
Sasa Ahly na TPM zinawania uongozi wa kundi ili kujihakikishia kutinga Nusu Fainali kabla ya mechi za mwisho za Kundi hilo, ambazo Ahly watamaliza na Zamalek Cairo na Mazembe watamaliza Berekum Chelsea nchini Ghana.

Post a Comment

Previous Post Next Post