SIMBA YATOKA SARE NA CITY STARS(AKUFFO AENDELEZA REKODI YA MABAO MSIMBAZI)

Akuffo 
SIMBA SC imelazimishwa sare ya 1-1 na City Stars ya Nairobi Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha jioni hii, katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na mechi ya Ngao ya jamii dhidi ya Azam FC, Septemba 11, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Simba imeshindwa kulipa kisasi cha Agosti 8, mwaka huu ilipochapwa mabao 3-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na timu hiyo.
Katika mchezo huo, bao la Simba lilifungwa na Daniel Akuffo, wakati Komabil Keita alijifunga katika jitihada za kuokoa na kuwapa Wakenya bao la kuongoza.

Post a Comment

Previous Post Next Post