SIMBA SC NA CITY STARS ARUSHA LEO

Simba SC
SIMBA SC leo inashuka kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha kumenyana na City Stars ya Nairobi, katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na mechi ya Ngao ya jamii dhidi ya Azam FC, Septemba 11, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hiyo itakuwa mechi ya pili kuzikutanisha timu hizo, awali Agosti 8, mwaka huu Simba ilichapwa mabao 3-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Lakini kufungwa huko kwa Simba kulitokana na kocha Mserbia Milovan Cirkovick, kubadilisha karibu kikosi kizima kilichoanza na kuingiza wachezaji wapya, ambao waliitoa City Stars ya Nairobi nyuma kwa 1-0 na kuipa ushindi wa 3-1.

Post a Comment

أحدث أقدم