WACHEZAJI 22 WALIOCHAGULIWA NA KOCHA MKUU WA YANG TOM SAINTFIET KWENDA MBEYA KESHO.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet ameteua wachezaji 22 kwa ajili ya mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, dhidi ya Prisons Jumamosi kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo makao makuu ya klabu, Saintfiet alisema ameteua wachezaji hao kulingana na mazingira ya mechi yenyewe na kwamba wachezaji wengine wote waliobaki ni wazuri pia.
Aliwataja wachezaji aliowateua ambao wanaondoka kesho asubuhi kuwa ni makipa; Yaw Berko, Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Shadrack Nsajigwa, Juma abdul, Godfrey Taita, Mbuyu Twite, Kevin Yondan,  Nadir Haroub ‘Cannavaro’, David Luhende, Oscar Joshua na Stefano Mwasyika.
Aliwataja viungo ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Rashid Gumbo, Nizar khalfan, Shamte Ally na Simon Msuva, wakati washambuliaji ni Jerry Tegete, Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi na Hamisi Kiiza.
Aliwataja wachezaji wa kikosi cha kwanza ambao hawatasafiri kwa ajili ya mechi hiyo kuwa ni kipa Said Mohamed, Ladislaus Mbogo, Job Ibrahim, Juma Seif ‘Kijiko’, Salum Telela, Omega Seme, Nurdin Bakari, Idrisa Assega na Issa Ngao wa Yanga B, ambaye anakomazwa kikosi cha kwanza.

Post a Comment

Previous Post Next Post