| Sanga akizungumza na Waandishi wa Habari mida hi. kulia ni Tito Osoro, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na kushoto Isaac Chanji, Mjumbe wa kuteuliwa |
![]() |
| Mkutano na Waandishi |
Na Mahmoud Zubeiry
UONGOZI
wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, umeisimamisha kazi Sekretarieti
nzima ya klabu, akiwemo Katibu Celestine Mwesigwa na Ofisa Habari, Louis
Sendeu, kutokana na kile ilichoeleza utendaji usioridhisha.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari ‘mida hii’ makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar
es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema kwamba
maamuzi hayo yamefuatia kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika
tangu saa 5:30 leo hadi saa 9:30.
Wengine
wanaokumbwa na panga hilo ni Masoud Saad, aliyekuwa Ofisa Utawala,
Philip Chifuka aliyekuwa Mhasibu na Hafidh Saleh aliyekuwa Meneja ambaye
anahamishiwa kwenye majukumu mengine.
“Tumesitisha
mikataba ya sekretarieti nzima, pia tumefanya marekebisho, tumemtoa
Meneja wa timu na muda si mrefu tutamtangaza Meneja mwingie pamoja na
sekretarieti mpya,”alisema Sanga.
Aidha, Sanga alisema Kocha Mbelgiji, Tom Saintfieti anapewa onyo kali kwa kuzungumza ovyo na vyombo vya habari.
“Tumekwishakutana
naye mara kadhaa kumpa utaratibu wa kuzungumza na vyombo vya habari,
sasa tutamuandikia barua ya kumkumbusha wajibu wake na kuzingatia wajibu
wake, kutozungumza na vyombo vya habari holela,”alisema.
Kwa
ujumla maamuzi haya yanakuja baada ya Yanga kuanza vibaya Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, ikiambulia pointi moja tu katika mechi zake mbili
za awali, kutokana na sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja
wa Sokoine mjini Mbeya Jumamosi na Jumatano ikachapwa mabao 3-0 Morogoro
Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Chanzo: bongostaz blog


إرسال تعليق