
.
Kwa yeyote anaefatilia
bongofleva toka kitambo kidogo najua jina la Matonya lazima litakua
kwenye list ya familia ya wanabongofleva.
Ni jina ambalo limekua kwenye
vichwa vya vizito vya habari mara kadhaa kutokana na stori kama ya
kukamatwa na dawa za kulevya Chinapamoja na stori nyingine.
Stori ya mwisho mimi kuisikia
na nikawa na hamu ya kuifahamu ni kuhusu taarifa kwamba msanii huyu
mzaliwa wa Tanga 96.0 amekwama kwenye ishu zake za maendeleo kwa sababu
kuna watu wanamloga asifanikiwe tena ikiwemo kukwamisha uzinduzi wa
hoteli yake aliyoijenga Tanga ambayo ilitakiwa kufunguliwa toka miezi
sita iliyopita.
Namkariri akisema “nilikua na
harakati hizo za kufungua hoteli lakini majukumu yalinizidi nguvu kidogo
lakini taratibu yangu iko palepale japo ile time niliyotarajia
haikufanikiwa lakini bado nina mpango huo japo sitotaja siku, kuhusu
ushirikina hiyo inasemekana lakini siwezi kusema ni kweli au sio kweli
kwa sababu hayo ni mazingira ambayo yametuzunguka, mazingira yetu sisi
waswahili”
“Siwezi kusemea swala hilo liko
vipi lakini kikubwa tunapigana kila siku sichoki kumuomba Mungu kwa
sababu siku zote penye mazuri hakukosi kuwa na mabaya kwa hiyo
yanayosemwa labda ni ya kweli au sio kweli” – Matonya
Hoteli yake ni ya vyumba 10 ambapo ina pub ndani yake.
إرسال تعليق