Msanii wa Bongo fleva, Naseeb Abdul, a.k.a Diamond wa wasafi siku za
hivi karibuni alifunguka na kusema kwamba hana mpango wa kuoa siku za
karibuni kwa kuwa bado anahitaji sana mapenzi ya karibu na mama yake.
Akihojiwa na vyombo vya habari hapa Tzee, Diamond alisema kumekuwa na
maneno mengi sana yanayozagaa kuwa hivi karibuni atamuanika mchumba wake
anayetaka kufunga naye ndoa, jambo ambalo si la kweli.
Diamond, ambaye unaweza kusema ndiye mwanamuziki anayefunika kwa sasa
katika miondoko ya Bongo fleva, kutokana na ngoma zake kupendwa na
mashabiki wengi hapa Tzee hata nje ya Tzee, alisema kwamba mbali na
kuhitaji mapenzi kwa mama yake, pia ushauri wake ni jambo la muhimu
katika kila jambo analotaka kulifanya.
“Unajua mimi ninampenda sana mama yangu na ndiye kila kitu kwangu, hivyo
najikuta hakuna kitu ninachoweza kufanya bila kumjulisha, hivyo kuwa
naye mbali kwa sasa itakuwa ngumu,” alisema.
Akizungumzia kuhusu uhusiano wake na aliyewahi kuwa na mahusiano na Miss
Tanzania 2006, Wema Sepetu, alisema kwa sasa ni rafiki yake wa kawaida
tu, si mpenzi na wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbalimbali.
Kwa mujibu wa Diamond, matatizo yote yaliyotokea huko nyuma,
wameshasameheana na sasa hivi wanaiva vilivyo.
Diamond na Wema walishawahi kuwa wapenzi na kujikuta wakimwagana
mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo habari zao ziliteka vyombo mbalimbali vya
habari, hasa pale mwanamuziki huyo alipofanya onesho lake Mlimani City
na kuzikataa fedha alizokuwa akipewa na mwanadada huyo.Lakini kwasasa
Diamond anatuhumiwa kwamba anamahusiano na mtu mwingine anayefahamika
kwa jina la Najma sema msanii aliendelea tu kusema kwamba Najma si
mpenzi wake ila ni rafiki tu Duuuuhh!!!!! baada ya hayo ndipo akaamua
kusma kwamba suala la kuoa sio wakati huu ni baadaye sanaa .

إرسال تعليق