Imeandikwa na Shabani Mtoi,
Tunapo kuwa tunajiuliza
mhemko wa udini unatoka wapi au nani wameusababisha na kuuasisi si
vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande wetu waislamu. Ukimjua adui ni
rahisi kupambana naye na ni nusu ya ushindi kwenye vita ya kutafuta haki
au usawa au kuondoa tunao uita unyanyasaji kwa waislamu au mfumo kristo
kama wengine wanavyo penda kuita (Mimi sio muumini wa dhana ya mfumo
kristo) maana nimeona wakati wote waislamu wenzangu wakishika nafasi
kubwa serikalini, kwenye mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.
Siuoni mfumo kristo kama
unavyoitwa au kama baadhi ya waislamu wenzangu wengine wanavyotaka
kuaminisha umma wa kiislamu juu ya hii dhana. Nasema sioni kwa kuwa bado
naamini katika uwezo na si mfumo kristo, si uoni kwa kuwa hii nchi niya
wakristo, wapagani, waislamu, wahindu na dini nyingine. Si uoni mfumo
kristo kwa kuwa nimeshuhudia watu kama kina omari mahita, na said mwema
wakiwa viongozi wa vyombo ambavyo mara kadhaa vimesababisha mauwaji ya
waislamu wenzetu na ndugu zetu wakristo pia. Mtanisamehe bure wenye
mtazamo tofauti na wangu lakini siuoni mfumo kristo nikimuangalia jk na
makamu wake, si uoni mfumo kristo nikimuangalia wajina wangu Mohamedi
sheini na sharif hamad, si uoni mfumo kristo nikimuangalia Chande othman
yule jaji mkuu na Othamani Rashidi mkurugenzi wa usalama wa taifa, si
uoni hata nikiungalia kwenye wizara na taasisi nyingine za serikali.
Wanao ongela mfumo kristo
hawana udhibitisho wa kutosha kuhalalisha madai yao ambayo kwa sasa
nayaita hayana mashiko bali yametawaliwa na ukame wa maono na kiangazi
cha fikra kinacho piga macho pazia mchana wa jua kali.
Kwa waislamu na wasio kuwa
waislamu, Lazima tutambue kuwa adui wa waislamu sio wakristo, wapagani,
wahindu,au dini nyingine zinazopatikana kwenye huu ulimwengu.
Lazima tujue kuwa sisi ni
ndugu tunaohitaji kuishi kwa upendo na kuvumiliana bila kuathiri imani
zetu, na ikitokea lazima tutafute njia za amani kupata suluhu.
Kwa mtazamo wangu hawa ndio maadui wakubwa wa uislamu kwa Tanzania.
1. Adui namba moja kwa
waislamu ni kutokuwa na mashule na vyuo vingi vyenye kutoa elimu bora
kwa vijana wa kiislamu na hata wale wa upande wa pili wanaokuja
kuitafuta elimu. Najua kuna watu watapinga sana lakini ukweli mchungu
lazima tuuseme ili tupate pa kuanzia, mtakuwa mashahidi hata shule
tulizo nazo hazifanyi vizuri sana kwenye mitihani ya kitaifa lakini pia
hata mashule yetu hayana mfumo wa kuandaa masheikh walio iva kwenye
elimu dunia na akhera. Mimi napendekeza harakati zetu ziwe kwenye
kujenga mashule ya viwango pamoja na kuajiri walimu bora bila kujali
dini zao ili kuwaandaa vijana bora wanao endana na kasi ya sayansi na
teknolojia kuelekea soko la ajira ya ushindani na pia viongozi bora wa
dini.
2. Ni kukubali kufanywa
nyezo ya ccm kupata uhalali wa kutawala kwa kura za waislamu. Lazima
tujue kuwa ccm wametutumia vya kutosha na kutudanganya vya kutosha, sasa
tuseme basi! Mfano:~ Wametudanganya swala la mahakama ya kadhi wakati
wa kampeni 2010 waislamu waliotaka tuwe na kadhi kwa kauli hadaa ya ccm
wakapiga kura za kuhadaiwa lakini baada ya matokeo wakatugeuka! Huku ni
kuonekana kuwa tu-malofa wa kudanganywa, tuunge mkono chama ambacho
hakita tugawa lakini pia ambacho hakita tugawa na kuharibu umoja wetu wa
kitaifa.
3.Bakwata imekuwa ni kama
taasisi ya ccm, wanamuweka wanaye taka wao. Lazima tupiganie bakwata
kiwe chombo huru cha waislamu na tuweke viongozi wenye maono mapana
tunao taka sisi sio ccm hii itasaidia kurejesha imani kwa bakwata.
Napendekeza Qualification ya kuongoza Bakwata iwe ni PhD kwa kuangalia
uwezo wa elimu akhera na elimu dunia lakini pia pamoja na uwezo wa
kuongoza na kusimamia mambo. Chuo kikuu cha mum kinaweza kusaidia
kuratibu kupatikana wataalamu na watendaji wengine wa bakwata ambao nao
kiwango cha chini cha kuanzia kiwe shahada moja na kuendelea.
4.Kutokufuata mafundisho ya
mtume. Mtume wetu Muhammad S. A. W alikuwa mwema, mwingi wa hekima na
busara. Lazima tuyafuate mafundisho yake na kukumbushana mema na
kukatazana mabaya, uislamu haujajengwa kwenye misingi ya uhasama,
vurugu, fujo, chuki na mambo mengine mabaya. Uislamu umejengwa kwenye
misingi ya usafi wa matendo mema, kumcha Mungu, ukarimu, na kuhurumia na
kuwajali wengine. Tukiyafanya haya tutawaepuka wale wanao utumia
uislamu wetu kama daraja ambalo baadae hutuchafua wote. Mfano wale walio
ingia kuchoma na kuvunja kanisa na kuiba sadaka, baadhi ya vifaa vya
kanisa na mikate.
“Uislamu ni unadhifu” hii ni
moja ya tafsiri ya hadithi za mtume wetu kipenzi Muhammad S. W. A.
Tuyafuate mafundisho yake kwa matendo ili tumuenzi kipenzi chetu.
Credit:- http://www.malkiory.com/
Post a Comment