Uongozi wa Hisia za Mwananchi unawatakia Waislamu wote duniani Sikukuu ya 'Iyd
Al-Adhw-haa ambayo husherekewa kati ya tarehe 10 hadi 13 ya mwezi wa
Dhul Hijjah wa Kalenda ya Kiislamu.
Tunawapa mkono wa kheri na fanaka katika sherehe hii ya eid. Kiongozi wa Hisia za Mwananchi na familia zao wana furaha kubwa katika siku
hii ambayo husherekewa kama kumbukumbu ya sadaka ya Ibrahim(Abrahamu)
ambaye kufatana na taarifa za Biblia na za QuRAN alikuwa tayari ya
kumchinja mwanawe kama sadaka kwa Allah,Lakini M/mungu alimzuia
asimchinje akampatia Kondoo badala yake. Habari zake katika Quran ziko Sura al- hajj aya 37.
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutaqabalie du'aa zetu na za Waislam wote duniani, Aamiyn.
Post a Comment