MMILIKI wa B-Band, Banana Zorro amefunguka la moyoni kuwa, mimba
aliyopata dada’ke, Maunda Zorro mwaka jana ilikuwa ikimkera hivyo
akamnunia.
Akisemezana
na kituo kimoja cha televisheni cha jijini Dar juzikati, Banana alisema
kuwa kwa kipindi kile hakutarajia kama mdogo wake angepata ujauzito
ndiyo maana baada ya kupata taarifa hiyo alikasirika.
“Kusema ukweli hata yeye baada ya kupata ujauzito hakuweza kuniambia
moja kwa moja, akamwambia mke wangu, nilikereka sana lakini nilimsamehe
baada ya kupata mtoto,” alisema Banana.
Post a Comment