![](http://3.bp.blogspot.com/-X99sE_Xo6BA/UIk7JIoDovI/AAAAAAAAPFI/z4whXuJLhhQ/s1600/size8.jpg)
Kumekuwa na mjadala mkali sana juu ya
kurudiana kwa wapenzi walioachana.Mjadala huu umevuta hisia za wengi
na kumfanya Msanii size 8 naye aeleze ya moyoni......
Kwa mujibu wa size 8, kujirudi kwa mpenzi wako uliyeachana naye ni kosa kubwa sana na ni maamuzi ambayo si sahihi.......
Yeye anaamini kuwa kuachana ni Maamuzi na siyo Hisiana Maamuzi hayo ni lazima yaangaliwe kwa kina zaidi.
"Kuachana ni
maamuzi na siyo hisia.Lazima ujiulize kwa kina kwanza, je ni kwa nini
mlifikia hatua mkaachana. Inawezekana wakati huo mwenzio alikuwa na mtu
na hivyo kukuona hufai.
Ameenda huko katumika
weeee!!!!...baada ya kuchoka sasa anataka mrudiane huku akikudanganya
kwa maneno mazuri eti aliondoka kimakosa au aliondoka na mwili, roho
bado iko na wewe.
Huo ni uongo.Na
hii ndo sababu inayonifanya niamini kuwa mkitengana hakuna kurudiana kwa
sababu angekuwa anakupenda naturally basi angevumila na asingekuwa
tayari kukuona ukiteseka na maumivu ya mapenzi"Alieleza Size 8 na kuongeza kuwa :
"Sina maana muwe maadui.ila zingatieni faragha na mipaka yenu.Msije mkajikuta mnafanya mapenzi ya maigizo.Kama ni salamu basi salam tu na si vinginevyo"
Post a Comment