Katibu Mkuu wa Baraza la maimamu na Wahubiri wa Kenya Sheikh Mohamed Dor akifikishwa katika mahakama ya Mombasa hapo tarehe 18 Oktoba ambako alishitakiwa kwa kuchochea vurugu. [Na AFP] |
Serikali ya Kenya imeweka miongozo mikali ya kikemea hatuba za chuki
wakati nchi inajitayarisha kufanya uchaguzi mkuu mwezi Machi.
Sheria hizo mpya, zinazoitwa "Miongozo ya Kuzuia Upelekaji wa Ujumbe wa
Siasa Usiotakiwa kupitia Mitandao ya Mawasiliano ya Elektroniki",
zilitangazwa mjini Nairobi siku ya Jumatano (tarehe 24 Oktoba).
Miongozo hiyo itasimamia ujumbe zinazotumwa kupitia simu za mikononi
pamoja na usambazaji wake katika mitandao ya kijamii ili kuhakikisha
hakuna ujumbe za kuchokoza au kushawishi unatumwa katika Twitter au
Facebook, alisema Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari na Mawasiliano Bitange
Ndemo.
Miongozo hiyo inawataka wanasiasa kupeleka maandiko ya ujumbe wa kampeni
zao na matangazo ya kisiasa kwa ajili ya kuchunguzwa angalau siku mbili
kabla haijatumwa, kusemwa au kutangazwa kwa umma.
Tume ya Taifa ya Maelewano na Maingiliano, Tume Huru ya Uchaguzi na
Mipaka, Tume ya Mawasiliano ya Kenya (CCK), polisi na sekta nzima ya
mawasiliano ya simu, ambazo zilitoa miongozo hiyo, zitasaidia ili
kuimarisha miuongozo hiyo, Ndemo alisema.
"Wale watakaokiuka kanuni hizi watapelekwa jela," Ndemo aliiambia
Sabahi. Alisema kuwa mtu yeyote atakayetuma ujumbe za kutishia,
kutukana, kunyanyasa na ujumbe za uchochezi zenye uwezo kuchochea chuki
za kikabila kwa kutumia simu za mikononi na wale wanaovunja sheria za
kisiasa watakabiliwa na adhabu ya faini ya shilingi milioni 1 (dola
11,700), muda wa jela hadi miaka mitatu, au yote mawili.
Ndemo alisema miongozo hiyo imekusudia kuzuia vurugu ambazo ziliikumba nchi baada ya uchaguzi wa raisi wa mwaka 2007.
Wanasiasa wakuu walishitakiwa kwa kuchochea vurugu katika uchaguzi wa
mwaka 2007, ambao ulisababisha vifo vya watu wanaokisiwa 1,200 na zaidi
ya watu 300,000 kukimbia makazi yao, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
"Kwa mujibu wa ripoti za kiintelijensia, vurugu za kisiasa ambazo
zilizikumba sehemu nyingi nchini mwaka 2007 na mwanzoni mwa mwaka 2008
kwa kiasi kikubwa zilisababishwa na matumizi ya lugha isiyokuwa ya
kuwajibika na ya uchochezi wakati wa kugombea na mara tu baada ya
uchaguzi," Ndemo alisema. "Ili kutumia vizuri jukwaa la simu za mikononi
na kuimarisha utamaduni wa kidemokrasia na kuzuia umwagaji damu,
imekuwa ni jambo la haraka kuweka kanuni hizi ili kulinda dhidi ya
usambazaji wa ujumbe za chuki."
Ndemo alisema kuwa utekelezaji wake utafanywa kuwa rahisi zaidi mwezi
ujao ambapo simu zote za mikononi zitaandikishwa na serikali.
"Miongozo hiyo pia inawataka wafadhiliwa wa ujumbe za kisiasa sio tu
kujitambulisha wenyewe bali pia kutia saini nyaraka zinazowaidhinisha
kutuma ujumbe hizo na kuhakikisha wajibu wao unafuata kanuni,"
Mkurugenzi wa CCK Francis Wangusi aliiambia Sabahi.
Miongozo hiyo pia itataka ujumbe wa maandshi uweze kutumwa tu baina ya
saa mbili asubuhi hadi saa 12 jioni, zikiwa zimetumika lugha za
Kiingereza na Kiswahili tu na sio katika lugha nyingine zozote
zinazotumiwa na jamii za makabila.
Mary Ombara, mjumbe wa Kamati Elekezi ya Taifa juu ya Usomaizi wa Vyombo
vya Habari, alisema kuwa miongozo hiyo inavitaka vyombo vyote vya
habari kuwatumia waandishi wa habari wataalamu tu katika kuendesha
majadiliano ya kisiasa au kuandika maoni juu ya matukio ya kisiasa
nchini.
Aliiambia Sabahi kuwa waandishi wa habari wataalamu wana kiwango kikubwa
cha busara na uwajibikaji na hii itazuia ripoti juu ya matamshi ya
uchochezi kutoka kwa wanasiasa. "Tutakuwa tukisimamia kwa makubaliano,"
alisema. "Hatutaki tukamatwe tukiwa hatukujitayarisha."
Chanzo: sabahionline.com/
Post a Comment