KABANGE TWITE AMFUATA PACHA WAKE MBUYU TWITE.


Wakati kiungo mwenye uwezo wa kucheza kama kiraka Mkongo         Mbuyu Twite akiendelea kutimiza wajibu wake wa kuitumikia klabu ya Yanga tena kwa kiwango safi, pacha wa kiungo huyo Kabange Twite amewasili nchini na jana alikuwepo katika uwanja wa Taifa akimshuhudia pacha wake Mbuyu akisukuma gozi na cha kufurahisha akifunga bao la kwanza katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting uwanja wa Taifa.
Akiongea na Rockersports Kabange amesema kimsingi amekuja nchini kumtembelea pacha wake ambaye amekuwa mbali naye kwa muda tangu ajiunge na Yanga.
Kama Itakumbukwa kabla ya kujiunga na Yanga Mbuyu  pamoja Kabange wote walikuwa wamemaliza mikataba yao na klabu ya APR ya Rwanda na moja ya masharti ya ndugu hao ilikuwa ni kujiunga na ama Simba au Yanga wakiwa pamoja vilabu ambavyo vilikuwa vitani kutaka saini zao kabla ya Mbuyu aliyekuwa kivutio katika michuano ya Kagame kujiunga na Yanga.
Akiongea na Rockersports Kabange amesema hayuko tayari kuzungumzia juu ya hilo licha ya kukiri kuwa safari yake ya kuja nchini ilikuwa chini ya mmoja wa kigogo wa klabu hiyo Abdalah Bin Kleb.
Rockersports ilikuwa ikifanya naye mazungumzo wakati akimsubiri Bin Kleb kabla ya Bin Kleb kufika na kuondoka naye katika ndinga la Kigogo huyo wa Yanga.

Post a Comment

Previous Post Next Post