KAMATI YA LIGI YAIONYA AFRICAN LYON KUHUSU BANGO LA 'WE BELIEVE IN 0777'

Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeipa onyo kali timu ya African Lyon kutokana na washabiki wake kuweka bango lililoandikwa ‘We believe in 0777’ kwenye mechi yake dhidi ya Azam iliyochezwa Oktoba 6 mwaka huu Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
 
Bango hilo ambalo si la mdhamini wa Ligi Kuu ya Vodacom halitakiwi kuonekana tena kwenye mechi ambazo African Lyon inacheza vinginevyo Kamati ya Ligi itachukua hatua kali dhidi ya timu hiyo.
 
Kamati ya Ligi imezikumbusha timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kuzingatia kanuni zinazotawala ligi hiyo ili iweze kuendeshwa kwa ufanisi

Post a Comment

أحدث أقدم