Na Bongo5:
Ni jambo lisilofikirika kwa urahisi katika vichwa vya watu wengi
lakini mdadisi mmoja wa mambo juzi alinipa mtihani ambao nimebidi
nijaribu kuwashirikisha ninyi wadau wetu, maana baada ya mdadisi huyo
kuuliza swali mbele ya washkaji zake mimi nikiwemo, mjadala ukawa mkali
sana kiasi cha muafaka kutopatikana kwa urahisi.
Swali alilohusisha mdadisi huyo(jina kapuni) ni Je siku hizi wanawake natural wamepotea?
Mada ilianza hivi baada ya hapo kila aina ya majibu yalitoka na muda
mwingine kuamsha taharuki, kila mtu akivutia katika pointi ama maoni
yake.
Baada ya tafakari ndefu siku ya jana nikapata baadhi ya mambo ambayo
naomba wasomaji wetu tuchangie kadiri tuwezavyo. Katika tafakuri yangu
nilianza kuwachambua akina dada ambao tupo nao karibu.
Nikianza na nilivyowajua baadhi yao wakati wakiwa bado vijana wadogo,
nikagundua kuna tofauti kubwa sana kati ya wakati ule na leo. Moja ya
mabadiliko ni pamoja na rangi na baadhi ya viungo katika ya miili yao.
Tofauti hizo zinaanzia kichwani. Nywele zilizokuwapo kichwani mwao
wakati ule sio nywele za sasa. Sasa kuna ma weaving, Less wigs, Rasta za
kusukia, nywele za ki Brazilian na ki Hindi na kila aina ya
vikorombwezo. Ukishuka chini kidogo karibu na jicho nyusi za sasa nazo
hazipo tena.
Sijui sababu kubwa iliyopelekea jambo hili kutokea na badala yake
mistari yenye rangi ime replace nyusi za dada zetu. Usishangae kuona
kope nyekundu, blue ama rangi ya dhahabu.
Na katika eneo hilo hilo kope za dada zetu siku hizi nazo zinachezewa
na kuongezewa mapambo. Ajabu na kweli.tukiwa bado tupo eneo hilo hilo
la kichwa tunashuka chini kidogo ni nadra kumkuta msichana siku hizi
ajapaka lipshine za aina mbali mbali ili kuongeza mvuto katika lips
zake.
Ukitoka hapo unabaki na kichwa chenyewe hapo sasa ndipo uhalisia kwa
asilimia kubwa unapokuwa haupo. Rangi ya kichwa, shingo, na sehemu
nyingine za mwili kama mikono na miguu zinapishana kweli kweli.
Siku
hizi ni lazima ujichubue ama uondokane na rangi yako uliyozaliwa nayo na
uonekane na muonekano wa Carolite ama vipodozi aina ya lotion.
Mtihani huo hata wanaume wamefeli pia siku hizi.
Ukiondokana na eneo la kichwa unashuka kwenye fahari ya kwanza ya
mwanamke ambayo ni maziwa. Siku hizi wanasema kuna hadi Brazilia za
kukuza matiti.
Suala hili limekuwa likiripotiwa katika magazeti ya udaku
kwamba dada zetu wanafanya kila aina ya jitihada alimradi wawe na
maziwa makubwa. Sijui maana yake ni nini hapo.
Ukitoka eneo hilo unashuka kwenye fahari ya pili ya mwanamke hapo
nazungumzia hips na makalio. Sasa hapo pia hali imekuwa tofauti maana
mchina ndiye anyehusika sana nadhani kwa eneo hili sitaongelea sana
kwani matokeo yake yapo wazi na kwa sababu mjadala wa suala hilo umekuwa
wazi sana.
Kikubwa ambacho kinaonekana kwenye makala hii ni kwamba dada wa kike
au mwanamke wa leo anatawaliwa na vikorombwezo vingi ku boost image,
mwonekano ama mvuto wake kiasi kwamba ukikutana na dada zetu unashangaa
kimetokea nini. Hata kucha sasa kuna acrylic nails sasa hapo ana nini
cha kwake maana kila mahali ana modification?
Hapa naomba nibalansi hii makala hatusemi kuwa mtu kupaka mafuta na
kushine ama kung’aa ni kuondokana na uhalisia. La hasha bali mwanamke wa
leo mathalani kuna sherehe basi tegemea kukutana vibweka. Mfano wa
harusi, ama kuna tukio la kijamii kama Miss Tanzania basi kazi kubwa
katika siku hiyo inafanyika saluni.
Na huko ndipo gereji za kuondoa ama kubadilisha uhalisia wa dada
zetu, maana spea na spana zote za kufanyia kazi hiyo zipo huko. Mi ni
kama yule mdadisi ambaye anasema ame miss mwanamke natural wa kitanzania
ya na si photocopy ya Rihanna ama Nicki Minaj.
إرسال تعليق